Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika amefariki dunia kwa mshuto wa
moyo akiwa Johannesbuerg nchini Afrika Kusini alipopelekwa kwa matibabu.
Akiwa
ameandamana na mkewe na jamaa zake wa karibu, rais huyo alisafirishwa
hadi Afrika kusini katika hali ya usiri mkubwa huku akiwa hana fahamu.
Hali iliyozua hofu na utata mkubwa nchini Malawi kwani kwa muda mrefu kumekuwa na shinikizo za kumtaka Mutharika ang’atuke.
Awali
afisa mmoja mkuu wa serikali ya Malawi alinukuliwa akisema kuwa Rais
Mutharika mwenye umri wa miaka 78 aliangua akiwa katika makaazi yake
rasmi na kupelekwa hospitalini ambako aliwekwa katika chumba cha
wagonjwa mahututi.
Kuhusu nani ataongoza taifa hilo fuatia kifo
cha rais huyo, kulingana na katiba ya Malawi, Makamu wake Bi Joyce Banda
atalazimika kushikilia hatamu za uongozi kwa kipindi kilichosalia .
Hata
hivyo Bi banda na rais Mutharika walikuwa hawasikilizani kwani
walikosana mwaka wa 2009 na Makamu huyo wa Rais akalazimika kuhamia
upinzani.
RIP MUTHARIKA.
No comments:
Post a Comment