Rais wa jamhuri ya Muungano Tanzania JAKAYA MRISHO
KIKWTE,ametoa zawadi za sikukuu ya
pasaka kwa wazee wanaolelewa katika kituo cha wazee Kilima Bukoiba vijijinji.
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais Kanali MASSAWE
amekabidhi zawadi hizo kwa niaba ya rais wa Jamhuri ya ya muungano Mh JAKAYA
MRISHO KIKWETE.
Rais KIKWETE ametoa kilo miamoja za mchele, lita 40 za
mafuta ya kula na mbuzi wawili kwa wazee hao kwa ajili ya kuwafariji katika
kusherehekea sikukuu ya Pasaka.
Amesema kuwa yuko nao bega kwa bega katika kuhakikisha
wanayamudu maisha waliyonayo, kwa kuwataka wasjione wapweke katika kipindi hiki
cha sikukuu pamoja kuahdi kuendelea kufuatilia maisha yao katika kituo hicho
cha kilima chenye wazee 15 wakiwemo wanaume 9 na wanawake 6, pamoja na watoto
yatima 13 wasiyojiweza.
Kanali MASSAWE amewataka viongozi wa kituo hicho kuandaa utaratibu wa kuwa na shamba la kituo ambalo litasaidia wazee hao baadhi wenye nguvu kujishughulisha ili kuweka afya zao katika hali nzuri ya kuchangamka.
Mkuu huyo wa mkoa, amekabidhi shilingi elfu 20 kwa mkuu wa
kituo hicho Bi CREMENTINA MARTINE kwa kuanzia kununulia majembe matano, ambapo
amemtaka mkuu huyo wa kituo kushirikiana na mtendaji wa eneo hilo kuandaa
utaratibu wa kuanzisha shmaba kwa kualika wadau mbalimbali ili washiriki
kuanzisha shamba hilo.
Ni mmoja wa wazee hao akiwa chumbani kwake kituoni hapo.
No comments:
Post a Comment