MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 9 April 2012

KIVUKO KILICHOAHIDIWA NA SERIKALI HAKIONEKANI;

Akizungumza na Blog hii Afisa tawala msaidizi miundombinu mkoani Kagera Bwana SEIF USSEIN, amesema kuwa utaratibu wa kujenga kivuko katika eneo la Rubafu kilomita 42 kutoka Bukoba mjini, katika eneo la Bugabo Bukoba vijijini, uliwekwa na serikali ya mkoa kwa mpango wa kurahisisha mawasiliano zaidi ya miaka miwili iliyopita.
 Amesema baada ya kuanza kujenga Ghati na kuikamilisha mambo yamekuwa magumu kwa maradi huo kusimamiwa na ofisi ya mkoa ikabidi kuiomba TANROADS mkoa ambayo ilikuwa katika mpango wa kukarabati barabara ya kwenda huko iwe kwa kiwango cha lami, hivyo pamoja na hiyo italazimika kuhamishia mradi huo kwa TANROADS baada ya kuonekana ni gharama kubwa ambazo itakuwa vigumu kuendeshwa na ofisi ya mkoa.
Nilipomhoji bwana Ussein kuhusu taarifa za mkandarasi kukatisha mkataba, alijibu kuwa ni kweli alikatisha baada ya serikali kumcheleweshea malipo lakini alilipwa kiasi flan cha pesa na bado anadai milioni 60 ambazo nilimuuliza kama amekatisha mkataba inakuwa serikali iendelee kumlipa badala ya yeye kuilipa serikali kwani ndiye aliyekatisha mkataba, alinijbu kuwa serikali haina hasara na hata hivyo hizo pesa mkandarasi huyo hajaja kuzidai.

Mapema nikizungumza na baadhi ya wafanyakazi waliokuwa kwenye kampuni ya mkandarasi kutoka kampuni ya JESCO ya jijini Mwanza iliyokuwa ikifanya kazi hiyo ikiwemo kujenga nyumba za wafanyakazi na TRA na Uhamiaji, walisema kuwa mkandarasi huyo ameshafariki lakini aliacha amekabidhi kila kitu.

Awali wakti nikichunguza uwepo wa kivuko hicho, nilifanikiwa kuelekea katika maeneo ya Kabindi na Kasensero nchini Uganda, nikakuta hakuna shughuli zozote za uwepo wa kivuko na nilipomhuliza afisa huyo alisema kuwa hata wao mapema walipata wasiwasi, lakini walishatuma barua kwa waziri wa uchukuzi ambaye alifanikiwa kukagua maeneo hayo alipofanya ziara mkoani Kagera na aliahidi kuliwasilisha kwa viongozi wa jumuiya ya afrika mashariki EAC kwani ni wazo zuri.

Hadi sasa ni miaka 2 tangua kuahidiwa kivuko hicho jambo lililozua maswali mengi kwa jamii ya wanakagera na baadhi ya wavuvi kutoka Uganda kwani hawaoni kinachoendelea, kwasasa majibu ndiyo hayo.

No comments: