Mwenyekiti huyu (PICHANI CHINI) anadai kuwa wamebaini asilimia 92 ni unyanyapaa kati ya viongozi na walemavu wilayani karagwe.
Pamoja na hiyo mwenyekiti huyo amesema kuwa wamekuta baadhi ya wanafunzi wanaotakiwa kulipiwa gharama za shule halipiwi na badala yake wanalipiwa watoto waviongozi, kama watoto wa diwani ndiyo wanaolipiwa.
Amesisitiza kuwa wanaofanya ubadhilifu huo ni wenyeviti wa vitongoji, watendaji wa kata na vijiji kwa kushirikiana na madiawani wa maeneo husika.
Chini ni Kizito malinzi aliyekuwa dereva lakini alipata ulemavu mwaka 2010 baada ya kuwa alikuwa akirekebisha gari na gafra mwenye nalo akaliondoa na kumgonga na kumsaga mguu, kwa mujibu wake kesi inaendelea lakini haisikilizwi kwa umakini kwani kila akifika anapewa tarehe na anafamilia ya watoto 6 lakini anaishi kwa kuomba omba kutokana na kukosa mtaji, lakini anaomba wa kumsaidia nyenzo za kushona viatu na zingine za mkono anaweza kuzifanya hivyo mwenye uwezo amsaidie.
Akizungumza nami mwenyekiti wa halmashauri ya Karagwe Bw Ishuju Lunyogoto, amesema hakuna ruzuku ya serikali lakini wao kama viongozi wameweka mpango wa kujenga shule tano zenye miundombinu ya kuwapokea walemavu.
No comments:
Post a Comment