Wakizungumza katika kuuaga mwili wa Kanumba waziri Nchimbi amesema kazi za wasanii sasa imefika ukomo kwani kutokana na maombi ya wasanii walioogozana na Kanumba mwaka jana waliomba kuwa na shirikisho litakalosimamia kazi zao na rais pamoja na viongozi wengine wamesema hii nafasi inatumika kusisitiza kuendeleza fani hii ambayo ilikuwa ikifanywa kwa makini na msanii STEVEN CHARLES KANUMBA.
Naye katibu wa kamati ya mazishi na msiba JB amesema kuwa Kanumba atakumbukwa sana katika fani hii si kwa tanzania pekee bali afrika mashariki na kati na dunia nzima. Bofya Video ili kusikia waziri Nchimbi na baadaye JB kwa walichokisema hivi punde.
No comments:
Post a Comment