
Akizungumza na wadau wa kilimo na biashara mkoani humo,
mtafiti wa mazao ya kilimo Bwana INNOCENT NDYETABULA, amesema kuwa wananchi
wakijikita kufanya kilimo cha viazi rishe kwa kufauata maelekezo ya wataalamu
watajipatia chakula cha kutosha na kukuza uchumi.
Bwa Ndyetabula amesema hayo kwenye mkutano wa uzinduzi wa
mradi wa viazi rishe utakaoendeshwa kwenye wilaya za Muleba na Misenyi mkoani
Kagera.
Naye mtaalamu wa vimelea vya magonjwa ya mimea Dokta
MAGDALENA WILLIUM, amewata wananchi kutobagua vyakula vya asili hasa viazi
rishe, kwani pamoja na kuongeza uchumi kwa wananchi, pia vinatibu magonjwa sugu
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment