Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu FABIEN
INYASI MASSAWE, amesema kuwa
asiyehesabiwa katika sense atajikosesha haki za msingi na huduma muhimu kutoka serikalini.
Hata hivyo Kanali Massawe amesema kuwa wananchi
wasikubali kufungua milango usiku kwani
zoezi la kuhesabu litafanyika mchana ili kuondoa mianya ya vibaka kufanya
uhalifu katika majumba ya watu.
Katika hatua nyingine Kanali Massawe, amewataka wananchi
kutokaribisha wahamiaji, kwani zoezi hili linakwenda sambamba na upataikanaji
wa vitambulisho vya makaazi, hivyo wahamiaji watataka kujipatia vitambulisho
hivyo kumbe si watanzania, hivyo atakayebainika atahukumiwa kwa mujibu wa
sheria.
Muandishi wa Habari wa Redio Vision Fm akimuuliza mkuu wa
mkoa swali kuhusu SENSA
No comments:
Post a Comment