Amesema viongozi wenye mamlaka ya kuwaongoza wananchi,
wametakiwa kusimamia majukumu yao ipasavyo ili kukuza maendeleo na kutimiza
sheria za nchi.
Akiongea katika mahojiano maalum na mwandishi wa kituo hiki,
Baba askofu msaidizi jimbo la Bukoba METHODIUS KILAIN, amesema kuwa ni muhimu
kuhakikisha kazi na majukumu waliopewa kila kiongozi yanatekelezeka kisheria
ili kuondoa mianya ya Rushwa.
Askofu KILAIN amesema kuwa atasimamia usemi wake na kulitaka
kanisa katoliki kuhubiri ukweli hata kama wakichukiwa na baadhi ya watendaji,
ilimradi watekeleze sheria na haki kwa wananchi.
Ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi
katika zoezi la sensa ya watu na makaazi linalotarajiwa kufanyika Agost 26
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment