MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday 27 August 2012

WAZIRI WA AFRIKA MASHARIKI SAMWEL SITTA, AWASILI KAGERA KWA ZIARA KATIKA MPAKA WA TANZANIA UGANDA, RWANDA NA BURUNDI

Baada ya kupokelewa na kupewa taarifa ya mkoa na mkuu wa mkoa huo Kanali mstaafu Fabian Massawe, waziri Sitta ameshauri mkoa huu kuanzisha masoko ya mifugo karibu na mipaka ili kupunguza uingiaji wa wahamiaji haramu nchini, kwani wengi wanaingia kwasababu ya kulisha mifugo pamoja na mila za kijamii.
Waziri Sitta ametoa kauli hiyo baada ya kupokea taarifa inayosema kuwa kwasasa mkoa una wahamiaji haramu 3500 ambapo sababu kubwa yao inatokana na wafugaji pamoja na wakulima kufuata na mila na desturi  ijulikanayo kama Nyarubanja System.
Hata hivyo Kanali Massawe amemwambia waziri huyo wa afrika mashariki, kusaidia uwezeshaji wa vyombo vya ulinzi na usalama kutokana na kukosa vitendea kazi muhimu.


Waziri SAMWEL SITTA ameanza ziara yake katika mpaka wa Tanzania na Uganda ulioko kilomita 70 kutoka Bukoba mjini eneo la Mtukura na ataelekea Karagwe, Ngara na Bihalamuro.
Viongozi wa ulinzi na usalama wakiwemo Mkuu wa wilaya ya Bukoba Zipora Lion Pangani, Mshauri wa mgambo mkoa, kamanda wa polisi mkoa, afisa msaidizi uhamiaji na Kamishna wa Magereza mkoa pamoja na waandishi wa habari wameshiriki mapokeo na kusikiliza uwasilishaji wa taarifa ya mkuu wa mkoa kwa waziri Sitta.

No comments: