Julius Malema amewaambia wafuasi wake kuwa katu hatishiki na
uamuzi wa mahakama kusema kuwa ana kesi ya kujibu.
Mahakama hii leo ilimwachilia kwa
dhamana Malema anayekabiliwa na shtaka la kuhaulisha pesa.
Malema ambaye aliwahutubia wafuasi
wake nje ya mahakama, pia anatuhumiwa kwa kutumia nafasi yake ya zamani kama
kiongozi wa tawi la vijana la ANC kujitajirisha yeye na washirika wake wa
biashara.
Washirika wake wengine wanne nao
walikabiliwa na mashtaka sawa na hiyo katika kesi yao iliyosikilizwa hapo jana.