
Wasukuma mkokoteni nao wameshiriki maandamano ya kuelekea sehemu maalum kwa ajili ya hotuba ya mgeni rasmi.
Cha kushangaza ni wanafunzi tu, walioonekana kujitokeza na kubeba mabango yenye ujumbe kama unavyoona kwenye picha juu na chini.
Mgeni rasmi kwenye maonesho hayo alikuwa mkuu huyo wa mkoa ambaye amesisitiza jamii kuzingatia sheria na taratibu za matumizi ya barabara ili kupunguza ajali zisizo za lazima, hata akavitaka vyombo vya usalama hasa wa barabarani kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi ya alama za barabarani.
Picha juu ni kutoka kulia ni mwenyekiti musalama barabarani YUSTO KABANTEGA, akifuatia mgeni rasmi katika maadhimisho mkuu wa mkoa FABIAN MASSAWE, RCO Bwana MATAGE, mkuu wa wilaya Bukoba Bi ZIPORA PANGANI na kushoto ni Kamishina Magereza YUSUPH KIMANJI.
Maadhimisho yamefunguliwa kwa maandamanao yaliyohusisha vyombo vya usafiri mbalimbali kutoka stendi kuu ya mabasi mjini Bukoba na kuhitimishwa kwenye uwanja wa Kaitaba.
No comments:
Post a Comment