Habari kamili inasema kuwa ananchi wa kijiji cha Luita
kata ya Rugu wilayani Karagwe wamelalamikia
utaratibu wa serikali ya wilaya hiyo unaotumiwa katika kuwahamisha katika
baadhi ya maeneo opereisheini
inayoendeshwa katika sehemu mbalimbali za mkoa kagera.
Baadhi ya wananchi niliofanya nao mahojiano, wameeleza zoezi hilo kutekerezwa kwa njia za vitisho ikiwa ni pamoja na kuchomewa nyumba zao ambapo zaidi ya
nyumba 20 zimeripotiwa kuchomwa moto mpaka sasa.
Miongoni mwa raia hao ni Kasiri Pascal aliyesema kuwa nyumba 16 zilizchomwa jana lakini naye Makaranga Makoye amethibitisha kuwa ni nyumba zaidi 20 hadi sasa, na wanasema kuwa pale kuna wanyambo, wanyarwanda na wasukuma lakini kwa mujibu wao wanaochomewa ni wasukuma.
Operesheni hiyo inaongozwa na mwenyekiti wa kijiji Silidion Mgenyi huku Polisi na Mgambo wakichoma nyumba bila kujali vifaa vya wananchi hao na hawana pa kulala hadi sasa.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya karagwe ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya
ulinzi na usalama ya wilaya DARY
RWEGASIRA amesema zoezi hilo ni halali na linatekelezeka kwa misingi ya
haki katika operesheni inayofanyika Karagwe, Muleba na Ngara.
No comments:
Post a Comment