Usiku wa kuamkia leo majira ya saa 8:00 za usiku katika eneo la
Nyegezi watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia makazi ya Wakili
wa kujitegemea Elias Hezron na kumpigwa risasi ya tumbo kisha kumpora
kompyuta yake ya mkononi (laptop), simu tatu ikiwemo moja ya mkewe na
kutokomea kusikojulikana.
Wakili Elias Hezron wa kampuni ya uwakili ya JURISTIC LAW CHAMBER
inayomilikiwa na Hon. Justice Nchalla, Outa & Hezron, Partiner
Advocte ya jijini Mwanza ambaye amelazwa katika hospitali ya rufaa ya
Bugando chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) ambapo hali yake inadaiwa
kuwa mbaya hivyo madaktari wanaendelea kumpatia tiba ili kuokoa maisha
yake.
Akizungumza na Clouds kwa njia ya simu kaka wa wakili huyo George
Hezron ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa Novemba 2 mwaka huu
majira ya usiku baada ya muda mfupi kukatika kwa umeme ambapo wakili
huyo akiwa na mkewe walisikia kishindo cha kuvunjwa geti na hatimaye
mlango kisha watu wawili wasiotambulika sura zao waliingia ndani huku
wengine wakionekana nje ya nyumba na kumtaka Bw. Elias kuwapatia
kompyuta yake ya mkononi, simu zake zote naye kukaidi agizo la watu hao.
"Baada ya kumuamuru na yeye kukataa kutii kuwapatia kompyuta ndipo
mmoja wa watu hao aliamua kumpiga na kitu kizito (nondo) kichwani naye
kumkaba mwenzake hali iliyopelekea purukushani na kumzidia nguvu
jambazi, ndipo mwenzake alipoamua kutoa silaha na kumfyatulia risasi
tumboni kisha kupora vitu walivyohitaji na kumwamuru mke wa wakili huyo
pia kuwapatia simu yake ya mkononi na kisha wakatokomea kusikojulikana"
Alieleza kwa masikitiko kaka wa wakili huyo.
Bw. George amefafanua kuwa baada ya kupora kompyuta hiyo na simu
hizo watu hao walitokomea bila kuchukuwa kitu kingine huku kompyuta
iliyochukuliwa ikionekana kuwa na kumbukumbu na nyaraka za kesi
mbalimbali ambazo wakili huyo amekuwa akizisimamia kwenye mahakama za
mkoa wa Mwanza na mikoa ya jirani hali inayoonyesha kuwa watu hao
walikuwa wamekusudia kupora nyaraka hizo.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Bi. Lilian Matola
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari polisi wanaendelea na
uchunguzi wa kina na chanzo cha tukio ikiwa ni pamoja na kuwasaka kwa
udi na uvumba watu walio husika.
Habari kwa hisani ya GSENGO.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment