Waandishi wa habari mkoani Kagera wametakiwa kwenda samabamba na
mabadiliko ya maisha ili kuleta
maendeleo katika jamii inayowazunguka.
Hayo yamesemwa na katibu wa baraza la habari Tanzania bwana Kajubi
Mkajanga, katika mkutano wa siku moja uliowahusisha waandishi na wadau
mbalimbali wa habari mkoani Kagera……….CAST………..
Amesema kuwa ni lazima muandishi awe miongoni mwa jamii inayohitaji
maendeleo kwa kushika kalamu na vifaa vyake vya sauti ili kufikisha ujumbe kwa
jamii husika, ili kubadili hali ngumu ya maisha lakini pia kuleta sura ya
uelewa kwa maslahi ya jamii husika na kuendana na mataifa mengine.
Bwana Mukajanga ameongeza kuwa kulingana na mabadiliko ya
sayansi na teknolojia, ni lazima waandishi nao wabadilike tofauti na waandishi
wa zamani ambao walikaa kwenye nafasi zao za kazi pasipokujihusisha na
kujichanganya na jamii wanayoihabarisha.
Mkutano wa Braza la habari Tanzania umefanyika katika manispaa
ya Bukoba, baada ya kuandaliwa na chama cha waandishi wa habari mkoani Kagera
KPC, ili kuzungumzia vikwazo na changamoto za uandishi habari mkoani humo kwa
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment