MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday, 6 November 2012

WAKATI UPIGAJI KURA MAREKAN UNAFANYIKA

Katika kijiji cha Babu anakochimbuka Rais Barack Obama nchini Kenya, amejitokeza Mpiga lamri au mganga wa kienyeji aliyejulkana kama John Dimo na kurusha magamba ya konokono na simbi, mifupa na vitu vingine ka tunguli akibashiri ushindi wa Obama.

Baada ya kutupa vitu vyake alivyoviita kete katika kijiji Kogelo, Dimo, amabaye amejitambulisha kuwa na umri wa miaka 105, amesema simbi nyeupe zilizosogea mbele zaidi wakati wa kurusha zinaoensha kuwa Obama atashinda kwa kura nyingi dhidi ya mpizani wake.
 

Wakai wapiga kura wanafanya tathmini kutumia teknolojia ya kisasa, Dimo anatumia tunguli. Obama anazaliwa na baba mweusi kutoka Kenya, na mama mzungu kutoka Kansas na ana ndugu watano nusu-kaka na nusu-dada.

Nusu-ndugu ambaye ni Malik Obama alisema Jumapili kuwa familia inaona hakuna sababu kwanini Obama hasichaguliwe kwa muhula wa pili.
 
Alikuwa akizungumza wakati wa mashindano ya michezo ya kila mwaka kwa heshima ya baba yao marehemu, Sr Barack Obama.

No comments: