Nicolaus Mac (None Association Movement) KWA MATANGAZO YA REDIO NA TV WASILIANA NASI KWA +255767814844- nicolausngaiza@gmail.com.
Tuesday, 19 March 2013
Monday, 18 March 2013
KAMATI YA MAUDHUI TCRA YAKUTANA NA BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI MWANZA.
Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Kamati
ya Maudhui toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Mzee. Walter Bugoya
kushoto kwenye mkutano wa ziara ya kamati hiyo uliofanyika leo ukumbi wa
Hotel Gold Crest mkoani Mwanza, pichani wengine kuanzia kulia ni Bi.
Eunice Mabagala, Eng. Lawi Odiero ambaye ni meneja wa kanda, Bw. Abdul
Ngalawa (mjumbe), na mwisho kabisa ni Joseph Mapunda (Mjumbe).
Picha juu ni Mjumbe wa Kamati ya Maudhui ya
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania Abdul Ngalawa akitoa mchango wake katika
mkutano kamati ya Maudhui ya TCRA na waandishi wa habari wa baadhi ya
vyombo mkoani Mwanza, uliofanyika leo ukumbi wa Hotel Gold Crest ,
Kamati hiyo imeundwa kwa mujibu wa sehemu ya 4 ibara ya 26 (1) ya sheria
namba 12 ya Mamlaka ya Mawasiliano ya mwaka 2003.
Picha juu ni baadhi ya waandishi wa habari wa kwanza kulia ni SITA TUMA . Picha ni kwa hisani ya G sengo.
TAARIFA NIZOPOKEA KAMANDA HUYU AMEAGA DUNIA
PROFESA ANNA TIBAIJUKA; WANANCHI WAPIMIWE ARDHI NAKUPEWA HATI ZA UMILIKI
Waziri Tibaijuka amesema kuwa wamefanya mazungumzo na waziri wa maliasili na utalii Balozi Hamis Kagasheki, na kukubalia kutenga eneo kwa ajili ya wafugaji wa ndani ya nchi, kwani wameonekana kunyanyaswa na wasimamizi wa ardhi mkoani Kagera hasa maeneo ya Karagwe, Bihalamuro na Muleba, huku wakionekana kuwakumbatia wanyarwanda.
Kwasasa manispaa ya Bukoba imepima zaidi ya viwanja 4800, na imefidia wananchi kadhaa, jambo ambalo Prof amelitilia shaka na akauliza swali kama Kigambo fidia kwa ekali moja ni milion141 kwa manispaa ni sh ngapi?
Thursday, 14 March 2013
KATIBU MKUU CHADEMA DK WILBROD SLAHA; CHADEMA TUMEZOEA KUSINGIZIWA.
Kauli ya Dokta Slaha imetolewa baada ya Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Chadema,Wilfred Lwakatare
jana alikamatwa, akahojiwa na kupekuliwa na polisi kwa tuhuma za uchochezi wa
uvunjifu wa amani.
Katibu huyo mkuu wa chama hicho, amesema kuwa tukio hilo limejitokeza baada ya wao Chadema kupata taarifa kuwa ameonekana kwenye mtandao wa U-TUBE katika tukio moja wapo la kumdhuru mtu, jambo ambalo amesema hivyo ni vitu vya kutengeneza kutoka na kukua kwa teknolojia.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema polisi walifika katika ofisi
za chama hicho Kinondoni jijini Dar es
Salaam na kuomba kuzungumza na Lwakatare, hivyo kwamujibu wa sheria mtu kuhojiwa ni suala la kawaida ikabidi wamtume mwanasheria wao ili awape taarifa zaidi kuhusiana na hilo kwa mujibu wa sheria.
Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso alipoongea na Gazeti la
Mwananchi jana, alisema kuwa Lwakatare alikamatwa kutokana na taarifa zilizopatikana
kutoka katika video kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akiwahamasisha
watu kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani au uhalifu. Alipoulizwa mahali na
lini alikamatwa Lwakatare, Senso alisema hilo
halijalishi, lakini jambo la msingi ni kwamba wako naye kwa ajili ya uchunguzi
na hakutaka kuweka bayana ni lini wangemwachia.
Siku nzima ya jana mitandao ilikuwa imetawaliwa na habari ya picha ya video ikimwonyesha Lwakatare akidaiwa kupanga mikakati ya kumteka Mhariri Mtendaji wa Mwananchi, Dennis Msacky. Lwakatare alionekana akitoa maelekezo kwa watu, ambao sura zao hazikuonekana, akiwataka kufuatilia nyendo za Msacky.
Alionyeshwa akiwataka watu hao kumkamata bila ya kumdhuru Msacky, lakini wamtupe mbali kama njia ya kumnyamazisha. Alikuwa anamtuhumu Msacky kama alikuwa anashirikiana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ili kukihujumu chama chao.
“Inabidi mfahamu nyendo za mtu huyu, kama anapenda vitu kama kutembea usiku au kinywaji anachokunywa,” alinukuliwa kwenye mtandao huo.
Pia anaonekana kwenye video hiyo akitoa mbinu mbalimbali za namna ya kufanya utekaji nyara.
Wakili wa Lwakatare alonga
Wakati akihojiwa na kupekuliwa, Lwakatare aliongozana na wakili wa kujitegemea, Nyaronyo Kicheere, ambaye alilieleza Mwananchi kuwa mteja wake alichukuliwa kutoka ofisini kwake kwenye Makao Makuu ya Chadema yaliyoko Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kicheere alidai kuwa hakuwa na uhakika kuwa Lwakatare alikamatwa muda gani ofisini kwake kwani yeye aliitwa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi saa 9.00 alasiri.Mwananchi, hata hivyo, lina taarifa kuwa Lwakatare alikamatwa na askari wanne saa 7.00 mchana na kupelekwa Makao Makuu ya Polisi.
Lwakatare, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CUF na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alipokamatwa alifuatana na maofisa kadhaa wa Chadema akiwamo Ofisa wa Ulinzi wa chama hicho, Hemed Sabula na Ofisa wa Mawasiliano aliyejulikana kwa jina moja tu la Karungebe.
Alichukuliwa ndani ya gari aina ya Land Cruiser na kupelekwa moja kwa moja Makao Makuu ya Jeshi la Polisi katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Mahojiano
Kicheere alisema Lwakatare alihojiwa kwa tuhuma za uchochezi ingawa alidai polisi hawakubainisha ni uchochezi upi.
Mahojiano hayo kwa Lwakatare yaliongozwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Obadia Jonas.
“Lwakatare alihojiwa kuanzia saa 9.00 alasiri hadi 9.55 jioni na tuhuma zilizomkabili ni uchochezi. Ila askari hawakuniambia ni uchochezi upi,” alieleza Kicheere. Alisema kuwa baada ya mahojiano yale waliamriwa kwenda nyumbani kwa Lwakatare kwa ajili ya upekuzi.
Lwakatare, ambaye anaishi eneo la Kimara King’ong’o jijini Dar es Salaam, alisindikizwa na askari saba walioongozwa na ACP Jonas. Katika msafara huo wa kwenda kupekua nyumbani kwake, maofisa wa Chadema walizuiwa kuongozana naye, isipokuwa mwanasheria wake, Kicheere, ndiye aliruhusiwa kuongozana naye.
“Tunavyoongea na wewe hivi sasa ni kwamba upekuzi unaendelea katika vyumba vya nyumba . Kwa sasa tuko ndani ya chumba chake cha kulala,” alieleza Kicheere.
Kicheere alisema upekuzi huo ulianza saa 10.30 jioni na ulilenga katika kutafuta nyaraka ambazo zingeweza kutumika kama ushahidi wa tuhuma hizo. Alisema kuwa baada ya kumalizika kwa upekuzi kilichokuwa kinatakiwa kufuata ni kuandikisha maelezo katika Kituo cha Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
“Hawa jamaa wanaendelea na upekuzi na hawajapata kitu chochote muda huu tunavyoongea na wewe. Ila tukimaliza tutarudi Kituo Kikuu cha Polisi kwa ajili ya kuandikisha maelezo,” aliongeza Kicheere.
chanzo mwananchina na redio one.
PAPA MPYA YAPATIKANA KANISA KATOLIKI
Ni Kadinali Jorge Mario Bergoglio wa Argentina aliyechaguliwa
kuwa Papa mpya wa Kanisa Katoliki.
Kadinali Bergoglio anakuwa mtu wa kwanza kutoka Amerika kusini kuchaguliwa
kuwa Papa. Mara tu baada ya kuchaguliwa
alichagua jina la Papa Francis I.Awali moshi mweupe ulishuhudiwa ukifuka kutoka bomba la kutolea moshi katika kanisa la Sistine Chapel na kufuatiwa na kengele kupigwa. Hii ilikuwa ni ishara kwa walimwengu kuwa makadinali ambao walianza mchakato wa kumchagua Papa mpya hatimae walikuwa wamefaulu katika kazi yao.
Kadinali Bergoglio anachukuwa mahali pa Papa Benedict XVI, ambaye alijiuzulu mwezi uliopita akisema hana nguvu na uwezo wa kuendelea kuliongoza Kanisa Katoliki.
Makadinali 115 wamekuwa faraghani tangu siku ya Jumanne alasiri na wakaanza mchakato wao kwa kupiga kura mara nne kwa siku.
Ilikuwa inahitajika kuwa angalau Makadinali 77 yaani theluthi-mbili wangeliweza kumpigia kura mmoja wao ili aweze kutangazwa kuwa Papa mpya.
Na kabla ya mchakato huo kuanza kulikuwa hakuna dalili za
kuonyesha nani angelichaguliwa.
Maelfu ya watu kutoka sehemu mbali mbali duniani walikwa wamekusanyika
katika ukumbi wa Kanisa la St Peter tangu siku ya Jumanne.Muda mfupi kabla ya Kadinali Bergoglio kujitokeza , maelfu ya watu walionekana wakikimbia kuelekea ukumbi wa St Peters ili kuweza kumshuhudia Papa mpya akitangazwa .
Papa Francis I ni nani?
Alizaliwa Mjini Buenos Aires huko Argentina mwaka1936.Papa Francis 1 ni mtu wa kwanza katika kipindi cha miaka elfu moja (1,000) kwa mtu kutoka nje ya bara la Ulaya kutawazwa kuwa papa wa Kanisa Katoliki.
Papa Francis 1 ni mwana wa Mtaliano aliyekuwa akifanya kazi katika shirika la gari Moshi kabla ya kuhamia nchini Argentina miaka ya zamani.
Kama kadinali wa Jimbo la Buenos Aires ,Kadinali Bergoglio amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Argentina.
Hata hivyo Kadinali Bergoglio anapendwa sana na wafuasi wa kanisa hilo huko Argentina na hasa watu maskini.
adinali Jorge Bergoglio, mwenye umri wa mwaka 76, kwa karibu miaka yake yote kama Kasisi amehudumu nyumbani kwao Argentina.
Kadinali huyo wa Jimbo la Buenos Aires inasemekana aliibuka nambari mbili wakati Papa Benedict alipochaguliwa mwaka 2005
Anaaminika kuwa na ujuzi mkubwa ambao wengi wanasema utamsaidia sana katika uongozi wake.
Katika maisha yake ya huduma kwa Kanisa Katoliki huko Amerika Kusini ambapo Kanisa Katoliki lina waumini wengi zaidi duniani, Kadinali Bergoglio ameibuka kuwa mtu anayependa sana udhabiti wa kisiasa katika nchi zilizo katika bara la Amerika Kusini.
Bergoglio anasifiwa kwa kuleta mageuzi makubwa katika Kanisa la Argentina huku katika eneo hilo la Amerika Kusini Kanisa bado linashikilia itikadi za kale.
Tuesday, 12 March 2013
SAMAHANI WATAZAMAJI KWA PICHA HIZI LAKINI NDIYO UKWELI, BAADA YA MAJAMBAZI 7 KUAWA NA POLISI MKOANI KAGERA
Amesema kuwa tukio hilo limetokea, baada ya wasamaria wema kuitaarifu polisi
kuhusu njama za majambazi hao kuuvamia mgodi wa Tulawaka.
Amesema kuwa polisi waliweka mtego, na katika
majibizano ya risasi, polisi imefanikiwa kuwaua majambazi saba, ambapo watano kati
yao, wanasadikiwa kuwa ni raia wa BURUNDI .
Amesema kuwa miili ya majambazi hayo imehifadhiwa katika
hoospitali ya wilaya ya Biharamulo, na amewataka wananchi kufika katika
hospitali hiyo kuwatambua majambazi hayo.
Kamanda KALANGI amesema polisi pia imefanikiwa kupata
silaha mbili za kivita aina ya SMG, risasi 156, magazine tano na mabomu matatu
ya kutupwa kwa mkono.
MWANA HARAKATI
Subscribe to:
Posts (Atom)