Gari limeanguka katika mteremko wa Katoma nje
kidogo ya mji wa Bukoba, lilikuwa na watu watatu, majeruhi wawili walitolewa na
kupelekwa hospitali ya mkoa
Mmoja anayedaiwa kuwa ni
mwanaume amefariki na mwili wake umenasa katika gari baada ya kulaliwa na gari
hilo, hadi picha hizi zinapigwa, njia za kunasua mwili huo chini ya gari
zilikuwa hazijafanikiwa.
Kama inavyoonekana
wananchi waliofika eneo hilo wapo wanauchungulia mwili huo ulionasa, na gari
halikutambulika haraka na mmiliki wake kwani waliotakiwa kusema ndiyo
waliojeruhiwa.
Siku moja kabla ya ajali
hii, imetokea ajali nyingine manispaa ya Bukoba katika eneo la Rwamishenye na
kusababisha kifo cha mtu mmoja na mwingine kukatika mguu, ikihusisha gari aina
ya CATER mali ya familia ya Mbagwa.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment