Taarifa zilizopo ni kwamba tukio limetokea kwenye saa tano asubuhi kwenye Kanisa Katoliki Olasiti Arusha ambapo lilikua linazinduliwa na mgeni rasmi ambae ni balozi wa Papa hapa Tanzania.
Inasemekana chanzo ni bomu la kurushwa na mtu ambae aliwasili kanisani hapo na kurusha hilo bomu muda mfupi tu baadae ambapo walioumia wamekimbizwa hospitali ya Mount Meru.
Taarifa za karibuni kabisa zinaeleza kuwa mtu mmoja amekufa
kwenye mripuko uliotokea katika ufunguzi wa kanisa la Katoliki la Olasiti,
kwenye kitongoje cha Arusha, Tanzania.
Watu kama 50 wamejeruhiwa.Makamo wa rais wa Tanzania, Dr. Mohamed Gharib Bilal amewasili Arusha kwenda kupeleka pole ya serikali kwa viongozi wa kanisa na majeruhi.
Dr. Bilal alisema serikali ya Tanzania itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa inawapata watu waliohusika na mripuko huo.
Mtu mmoja amekamatwa lakini haikuelezwa ni nani au kama amehusika na kundi
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment