MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 6 May 2013

MAFURIKO BUKOBA......

Mkuu wa wilaya ya Bukoba bi ZIPORAH PANGANI, ametoa taadhari kuwa watu watakaoendelea kukaa kwenye makazi yao selikari inawatoa kwa nguvu kwani wameshaambiwa wahame maeneo ya mabondeni hawataki.

Wakati huo wakazi wa Kyabitembe na Nshambya wameshindwa kuvuka kupitia Rwamishenye baada ya daraja walilokuwa wakitumia kusombwa na maji ya mvua zilizonyesha usiku kucha na kupelekea
Wananchi wa eneo hilo manispaa ya Bukoba, waishi kwa wasiwasi baada yam to kanoni unawaunganisha na kata ya rwamishenye, kujaa maji wakati hakuna daraja mbadala la kuvukia kufuata huduma muhimu.

Wakizungumza na harakati kwa nyakati tofauti, wananchi wameskitishwa na njia iliyowekwa kama daraja la kuvukia huku ikionekana itadondoka dakika yoyote ilihali ikiwa tishio kwa watoto na kulazimu wazazi kusubiria taarifa yoyote kuhusu watoto waliokwenda shule.

Wamesema kuwa wakati mwingine watoto wanashindwa kwenda shule wakihofia kudumbukia majini na kusababisha kukwamisha upatikanaji wa elimu.

Mto kanoni katika eneo hilo, unatenganisha kyabitembe n6a6 r6wamis6hen6y6e, ambapo hu6tum6ik6a na wananchi hasa wanafunzi wa shule za rwamishasha, na omumwani na maeneo mengine kama sokoni.
.
Biashara zimesimama ghafla katika mji huo wa Bukoba na taarifa za serikali zinaendelea kutolewa kupitia redio za mjini Bukoba.


MWANA HARAKATI

No comments: