Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumatatu, Mei 6, 2013, ameamua kukatiza ziara yake ya Kiserikali nchini Kuwait ili
kurejea nyumbani kutokana na tukio la shambulio la kigaidi la mlipuko mjini
Arusha ambako watu wawili wamefariki na 60 wamejeruhiwa.
Rais Kikwete aliyekuwa aondoke kesho kurejea
nyumbani, amelazimika kukatiza ziara hiyo na anaondoka Kuwait
City kurejea nyumbani mara moja ili
kuwa karibu na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi.
Miongoni mwa shughuli ambazo hazitafanyika
sasa kutokana na uamuzi huo wa Rais ni ziara ya kutembelea Kampuni ya Mafuta ya
Kuwait katika eneo la Ahmadi mjini Kuwait. Aidha,
Rais hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni ambacho alikuwa anaandaliwa na
Waziri Mkuu wa Kuwait,
Mheshimiwa Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment