TAKUKURU yaitaka jamii imetakiwa kuelewa kuwa kuporomoka kwa maadili
kunasababisha uwepo wa rushwa nchini.
AFISA MKUU TAKUKURU MKOANI KAGERA AKIZUNGUMZA NAMI
Mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU,
Bwana JOSEPH MWAISWELO, katika semina maalumu ya maadili kwa wazee wa manispaa
ya Bukoba, katika mpango wa taasisi hiyo nchi nzima kuhakikisha waelimisha
kuhusu maadili ambapo mwaka huu wameanza na wazee.
Amesema
kuwa pamoja na maadili, umasikini pia unasababisha kuongezeka kwa rushwa hivyo
TAKUKURU imetambua hayo na kuamua kuanza na wazee ambapo pia wanashughulika na
wanafunzi wa shule za msingi
Bwana Mwaiswelo amesema kuwa rushwa nchini inaongezeka,
hivyo jamii itambue kuwa ni lazima maadili yazingatiwe, huku baadhi ya wazee
waliopewa semina hiyo na kutoa michango yao, ni pamoja na shekh wa mkoa ARUN
KICHWABUTA,(hayupo pichani) aliyesisitiza kuwa malezi bora ndiyo njia pekee ya kusaidia kizazi
cha sasa, ambapo amewata wazazi na walezi, kuwapa ushirikiano wa kutosha walimu
kuhusu watoto wao.
Katibu wa CCM manispaa ya Bi JANET KAYANDA,(hayupo pichani) kwa upande wake
amesema kuwa jambo la maadili siyo nla sekta Fulani, bali serikali madarakani,
wanasiasa na wataalamu pamoja na mwananchi mmoja mmoja wanatakiwa kushirikiana
pamoja, kwani akili inaendana na maadili.
MWANA HARAKATI