Mkuu wa mkoa wa kagera kanali mstaafu
FABIAN MASAWE amewataka wawekezaji wa nje na wa ndani kuja kuwekeza katika mkoa wa kagera kwani bado una fursa nyingi
za uwekezaji katika mambo mbalimbali ya kiuchumi ,utalii,elimu afya pamoja na
uvuvi.
Kanali amsawe ametoa rai wakati
akiongea na waandishi wa habari .
Amesema kuwa katika
mkoa wa kagaera bado kunahitajika uwekezaji katika zahanati ambapo mpaka sasa
hivi mkoa wa kagera una jumla ya zahanati 269 vituo vya afya 30 na vituo vya
afya kumi na tano.
Aidha kanali masawe ameongeza kuwa
kutokana na umuhimu wa faya kwa wananchi wawekezaji hawanabudi kuongeza
zahanati pamoja na hospital ili kuongeza upatikanaji wa huduma kwa karibu.
Kanali masawe ameongeza kuwa katika kongamano hilo wamewashirikisha
wawekezaji wa ndani na nje katika kusaidiana na serikali kutangaza furs
zilizopo hapa mkoani kagera.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment