Akizungumza katika Mdahalo ulio andaliwa na
asasi isiyo ya kiserikali (CHANGONET) Afisa tarafa wa wilaya ya Chamwino bwana
Mohamed Mtaki amesema wananchi wanatakiwa kufahamu haki pamoja na usawa dhidi
ya wanawake na walemavu.
Aidha bwana mtaki amesema katika jamii
kunabaadhi ya makundi ambayo yanaamini kuwa wanawake hawana haki ya kumiliki na
kusimamia haki na hiyo ni mila potofu katika jamii.
Nae afisa maendeleo ya jamii wilayani Chamwino
Bi Jaina Msangi amesema katika mgawanyiko wa rasiliamali wanawake wengi
wamekuwa hawapewi kipaumbele licha ya kuwa wao ni mchango mkubwa katika
jamii.
Kwa upande wa wananchi wa kijiji cha mlodaa wamekiri kuwepo kwa
unyanyasaji wa kijinsia katika kijiji chao na kusema kuwa
wanahitaji elimu ili kubadilika.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment