Imeelezwa kuwa Demokrasia
vijijini itapatikana iwapo vyombo vya habari jamii vitatumika kikamilifu na
kutekeleza wajibu wake wa kupasha habari kwa kutumia teknolojia mpya na hasa
simu.
Akifungua mafunzo ya wiki
moja katika Ukumbi wa Mazingira, Kibaoni Ifakara mkoani Morogoro, yanayowashirikisha
wanahabari jamii kutoka Pemba, Unguja, Pangani, Ifakara na Kyela, Mkuu wa
Wilaya ya Kilombero Hassan Masala hayupo pichani, amesema mbinu za kisasa zinahitajika
kuelimisha jamii na kupambanua mambo gani yafanyike ili kupata uongozi bora
vijijini na taifa kwa ujumla.
Baadhi ya waandishi na washiriki wa mafunzo hayo, wakifanya mazoezi ya pamoja jinsi ya matumizi ya simu katika kupashana habari.
Kulia ni Mkufunzi kutoka
UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu.
MWANA HARAKATI



No comments:
Post a Comment