Polisi Visiwani Zanzibar wamethibitisha kutokea milipuko mitatu ya
mabomu kati ya Jumapili na Jumatatu leo mchana visiwani humo.
Akizungumza na mwandishi wetu Erick David Nampesya, mkuu wa Polisi
Zanzibar, Hamdan Omar Makame amesema milipuko miwili imetokea leo katika eneo
la mgahawa wa Mercury huku mlipuko mwingine ukiwa umetokea katika eneo la
Mkunazini, ikifuatia mlipuko uliotokea jana Jumapili katika eneo la Pangawe.(Hudugu)
Mkuu huyo wa Polisi Zanzibar amesema kuwa hakuna vifo wala
majeruhi katika matukio yote matatu wala mali iliyoharibiwa, isipokuwa madhara
ya kisaikolojia kutokana na hofu na taharuki kutokana na matukio hayo.
Aidha mkuu huyo wa Polisi ameeleza kuwa upelezi unaendelea ili
kuwabaini waliohusika katika matukio hayo ingawa hadi wakati huu hakuna mtu au
mshukiwa yeyote aliyekwishamatwa kuhusiana na matukio hayo.
Kuhusu hatua za tahadhari kufuatia matukio hayo Kamanda Makame
amesema Polisi wanaendelea kuimarisha ulinzi katika sehemu mbali mbali visiwani
humo ikiwa ni pamoja na kufanya doria katika maeneo kadhaa na amewaondoa hofu
wananchi wa visiwa hivyo kuhusu usalama wao
CHANZO BBC
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment