MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 13 February 2014

MKUU WA MKOA WA DODOMA- REDIO NI KIUNGO MUHIMU KATKA MAISHA

 Kabla ya hotuba yake hiyo, meneja wa maadili wa MCT bwana ALLAN LAWA, amesema kuna kila sababu ya kuenzi redio zetu nchini kwani zinaweza kubadili hali ya taifa na mataifa mbalimbali kwa muda mfupi sana.
 Naye katibu wa MCT Kajubi Mkajanga, amesema kuwa redio inamfikia kila mmoja kwa kiwango chochote bila kujali maskini wala tajiri kutokana na kuwa haina kiwango au gharama kubwa.
 Bi rehema nchinimbi, amesema kuwa redio iliaminika sana wakati ule lakini kwasasa kuna mapungufu madogomadogo ambayo hasa yawezekana yanaletwa na ushindani wa kibiashara, hivyo wataalamu wasiichukulie kama mzaha kwani yaweza kuhatarisha amani na kushindwa kuwawezesha wanawake kama ilivyo kaulimbiu ya mwaka huu.

 Picha juu wa kwanza kulia ni Bi EDDA SANGA, mkongwe katika tasnia ya habari, akifuatilia kwa karibu hotuba ya mgeni rasmi na chini ni wanahabari mbalimbali wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi.

Haya ni maadhimisho ya tatu ya siku ya redio duniani, ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni tusherekehe ushiriki wa wananwake katika redio na wote wanaowawezesha.

Maadhimisho haya yanafanyika kwa mara ya kwanza mkoani Dodoma ambapo mwaka jana yalifanyika Dar es salaam.
MWANA HARAKATI

No comments: