
Wakizungumza kwa machungu kupitia maandalizi ya kipindi cha redio cha MBONI YA JICHO, kinachorushwa kupitia 88.5 Kasibante fm Bukoba, vijana hao wanaojishughulisha na kazi mbalimbali za kubeba abiria, kufyatua tofali, kulima na kubeba mizigo, wamesema wanajisikia vibaya kusikia vijana wenzao wa mjini wanafikiwa na kuungwa mkono na viongozi wao.


Hapa ni katika eneo la Gera Kiziba Misenyi, Bukongo kata Karabagaine, na Mwanzo mgumu Katoma, ambapo kwa pamoja changamoto kubwa ni mtaji mdogo kwa vijana hivyo wanaomba kuungwa mkono na viongozi wao hasa wabunge.
Pichani juu ni Mac Ngaiza nikiwa katika moja ya sehemu za ufyatuaji tofali baada ya kuzungumza na vijana wanaojishughulisha na kazi hiyo.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment