| Lugano Mwambuja alivyojeruhiwa |
| Beatrice Lusamba |
Mwanamke mmoja Mkazi wa Mtaa wa
Ilembo kata ya Iyela Jijini Mbeya amemjeruhi mume wake baada ya
kumwagia mafuta ya moto kichwani kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mgogoro wa ndoa
baina yao.
Mwanamke huyo aliyefahamika kwa jina
la Beatrice Lusamba (37) alitenda tukio hilo mwishoni mwa wiki majira ya saa
saba mchana ambapo alimwagia mafuta hayo Mume wake Lugano Mwambuja(50) ambaye
ni mwalimu wa Shule ya Sekondari Sange iliyopo Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya.
Akizungumzia tukio hilo Mhanga wa
kisa hicho alisema yeye makazi yake yako Wilayani Ileje lakini Mkewe pamoja na
baadhi ya watoto wake huishi Jijini Mbeya hivyo hufika nyumbani hapo mara
chache kwa ajili ya kutembelea familia na kupeleka huduma mbali mbali kama baba
wa familia.
alisema siku ya tukio alialikwa na
Mkewe huyo kula chakula cha mchana ambapo baada ya kukaribishwa ndani mwanamke
huyo aliingia jikoni akiwa na mayai matatu na galoni la mafuta ya kupikia, ambapo
yeye alibaki Sebureni akisubiri chakula alichokaribishwa apikiwe.
Alisema baada ya dakika kumi Mkewe
huyo alirejea Sebuleni akiwa ameshika kikombe chenye mafuta yaliyochemshwa
ambayo alimwagia mwilini na kisha kukimbilia nje akimwacha mumewe akiugulia
maumivu makali yaliyotokana na kuungua na mafuta ya moto mwilini mwake.
Mwalimu huyo aliongeza kuwa baada ya
kupiga kelele ya kuomba msaada ndipo alipojitokeza jirani yake aliyefahamika
kwa jina la Andamisye Kajange ambaye baada ya kumuona katika hali hiyo
alimkimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya alikopatiwa matibabu na
kuruhusiwa.
Mjumbe wa Mtaa Ilembo, Philly
Mwakapimba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa kabla ya
kupeleka Hospitali Mhanga waliripoti Kituo cha Polisi na kupewa fomu namba tatu
(PF3) pamoja na kufungua faili namba IR/2253/2014 na kuendelea kutibiwa.
Aliongeza kuwa mtuhumiwa hajakamatwa
hadi leo baada ya kutorokea kusikojulikana huku lawama likipewa Jeshi la Polisi
kutokana na kushindwa kumkamata mtuhumiwa kwa wakati hadi anapata mwanya wa
kutoweka katika eneo la tukio.
Akizungumzia mahusiano yake na mkewe
Mwalimu huyo alisema alioana na mkewe mwaka 2007 kwa ndoa ya kimila baada ya
kufiwa na mkewe wa awali mwaka 2006 alimyemwachia watoto wawili ambao ni
Doris(20) na Happy Mwambuja(21) ambapo aliamua kuoa mke huyo kwa ajili ya
kusaidia malezi ya watoto hao.
Alisema akiwa kazini mara nyingi
alikuwa akipata taarifa za mgogoro kati ya mkewe huyo na watoto jambo
lililosababisha usuluhishi wa mara kwa mara kufanyika ukiongozwa na Serikali ya
Mtaa huku sababu ikibainika kuwa ni tamaa ya mwanamke huyo kutaka kumiliki
Nyumba ya Mwalimu huyo ili iwe mikononi mwake na siyo Familia.
Mwanamke huyo
amekuwa akijaribu kuiba hati ya nyumba ili abadilishe majina na umiliki lakini
anashindwa hali iliyoml;azimu Mwalimu huyo kuamua kununua eneo lingine na
kujenga ili kumtengnisha mkewe pamoja na watoto lakini hali bado ilikuwa tete
baada ya mwanamke huyo kutaka amilikishwe yeye nyumba.
Mwalimu huyo anaendelea
kupatiwa matibabu Nyumbani kwake huku Jeshi la Polisi likiendelea kumsaka
mtuhumiwa kwa ajili ya kumfikisha katika vyombo vya sheria kujibu shtaka la
kujeruhi kwa makusudi.
mwisho.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment