| Pichani wananchi wakiuangalia mwili wa marehemu Mzee mmoja ambaye anatajwa kwa jina la Mihayo Ngofa aliyefariki dunia papo hapo juzi |
|
Marehemu Mihayo Ngofa anaye
kadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 65 hadi 70 aligongwa na daladala ya
kwanza iliyokuwa ikitokea mjini kati kuelekea Igoma na kisha kugongwa na
daladala nyingine ambapo zote zilikuwa zikipishana kwa wakati mmoja nyingine
ikitokea Igoma kuelekea mjini kati.
Mara baada ya tukio hilo daladala
hizo hazikusimama ziliunganisha safari zake kwa mwendo wa kasi bila
kufahamika zilipoishia.
Vielelezo vinaonyesha kuwa
marehemu alikuwa akitoka sokoni kuinunulia mboga familia yake.
Tukio hili linatokea wakati
Wakandarasi wa wa ujenzi wa daraja la kivuko kipya cha juu cha watembea kwa
miguu kikiwa katika hatua zake za mwisho kukamilika na kuanza kutumika.
|
PICHA NA ZEPHANIA MANDIA
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment