MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 20 March 2014

MTANDAO MPYA WA MAWASILIANO TANZANIA

Machi 19, 2014 Shirika la kuhamasisha viwanda (IPS), chombo na silaha ya maendeleo ya viwanda chini ya mfuko wa maendeleo ya uchumi wa Aga Khan (AKFED),jana wametangaza kuingia katika soko la mawasiliano la Afrika Mashariki chini ya kampuni iitwayo SMART. 
Pazia likishushwa kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa kampuni hiyo ya simu za mikononi-Smart."lets talk.                                     

Viongozi wakuu wa kampuni ya Smart Telecom,Afrika Masharikii wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washindi waliojipatia zawadi kupitia mtandao huo,baada ya kushiriki kwenye kampeni ya GIVE US A NAME iliofanyika hivi karibuni.


Jina la kampuni ni matokeo ya kura zilizopigwa Afrika Mashariki katika kampeni ya Uvumbuzi. Kuzinduliwa kwa kampuni hiyo kutaisaidia AKFED kukuza huduma zake za kibiashara kwa jamii katika nchi za Burundi, Tanzania na Uganda, lengo kuu likiwa kuwekeza na kuwahudumia wateja

Mtandao wa IPS una uwanda/uelewa mpana katika sekta ya mawasiliano. Ni washirika wakubwa wa Roshan shirika linaloongoza katika utoaji wa huduma za mawasiliano nchini Afghanistan na pia washirika muhimu katika shirika la Tcell linaloongoza katika kutoa huduma Tajikistan. 

IPS pia ni wawekezaji wakubwa na wa pekee waliowekeza SEACOM submarine cable venture in East Africa. Wakati umefika ambao ushirika wa IPS ndani ya SMART utaleta ushirikiano na kuweka record ya ushirikiano wa makampuni ya simu Nepal na Cambodia  na kuwafanya wawe waongozaji katika soko hili.

Kuzinduliwa kwa SMART kutashirikisha uzoefu wa AKDEF katika kuwekeza kwa lengo la kuhamasisha ujasiliamali na ujenzi wa uchumi wa sauti ambao utatoa fursa nyingi za ajira na kuboresha maisha ya watu. Afrika Mashariki. AKFED imewekeza Serena Hotels, Diamond Trust Bank, Jubilee Insurance Group, National Media Group na katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji na miundombinu kama vituo vya nguvu ya umeme vya Bujagali na Tsavo.

Na Mwanaharakati.

No comments: