Ni siku moja kabla rais huyo hajalihutubia bunge maalumu la katiba hapo kesho saa 10 jioni.
Rais Kikwete amewasili Dodoma leo jioni, ambapo kwa mujibu wa taratibu rais ukutana na baraza la mawaziri kabla ya shughuli za kuhutubia kuanza, ambapo kesho wabunge wa bunge maalum, wametakiwa kufika katika viwanja vya bunge hilo sa8 mchana.
Akihalisha bunge hilo muda mfupi uliopita, makamu mwenyekiti wa bunge maalumu SAMIA SLUHU, amesema kesho asubuhi hakutakuwa na shughuli yoyote, hivyo wajumbe wote wakutane saa nane mchana.
Leo mwanasheria maarufu kutoka Kenya Mh WAKO, amelihutubia bunge hilo, katika semina ya kuelezea masuala ya kikatiba, ambapo mh Kingune Ngubale Mwilu, amesema katiba inatakiwa kuangali uchumi ukowapi na ufike wapi kuboresha maisha.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment