Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa shilingi billion 8.2 kwa mkoa wa
Kagera ili kuhakikisha wananchi wa mkoa huu wanapata maji safi na salaama na yenye
uhakika katika maeneo yao hususani maeneo ya vijijini ifikapo 2015.
Mkuu wa mkoa ameta
kauli hiyo na kuzindua wiki ya maji Mkoani Kagrera tarehe 17/03/2014 katika
Manispaa ya Bukoba, kuadhimisha wiki ya maji anatembelea na kukagua miradi ya
Maji inayotekelezwa katika Halmashauri
za Wilaya zote za mkoa wa Kagera
Alizindua wiki ya Maji alitembelea
na kukagua mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira unaofadhiliwa na serikali ya
Ufaransa kupitia Shirika lake la Maendeleo la (AfD) unaotekelezwa katika Manispaa ya Bukoba kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania na
Mamlaka ya Majisafi na Maji taka Bukoba.
Mradi huo utakaogharimu
Shilingi billion 27,528,304,236 tayari umetekelezwa
kwa asilimia 30 na bado unaendelea kujengwa na Kampuni ya kutoka India
(Technofab-Gammorn-Toddy Joint Venture) na Msimamizi / Mshauri (Consultant) ni Laymer GKW Consult kutoka
Ujerumani.
Baada ya mradi huo kuwa
umekamilika unatarajia kutoa hudum ya maji katika kata 4 za Buhembe, Kagondo,
Kahororo na Nyanga ambazo zikuwa hazipati huduma ya maji na kukamilisha huduma
hiyo katika kata 14 ambapo wananchi watapata
maji kwa asilimia 90 kutoka
asilimia 75 za awali.
Pamoja na Mradi huo
Manispaa ya Bukoba pia itanufaika na Miradi mingine mitatu ambayoni : Mradi wa
Ujenzi wa Mfumo wa Kutibu Maji taka eneo la Nyanga. Mradi wa Mfumo wa majitaka (Kwaajili
ya eneo la Kati la mji wa Bukoba)
utakaogharimu EURO 226,675 na unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia LVEMP II
Pia mradi wa tatu ni wa
Maji katika miji mikuu ya Wilaya 6 (Biharamulo, Bunazi/ Kyaka, Chato, Kayanga/Omurushak
, Muleba na Ngara) na mradi huo utagharimu kiasi cha USD 817,800 na
unafadhiliwa na Benki ya Dunia ikishirikiana na Serikali ya Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera
anaendele na ziara ya kukagua miradi ya maji wilayani ambapo katika Wilaya ya
Missenyi alitembelea na kukagua ujenzi wa Mradiwa Majia katika kijiji cha
Rukulungo wenye gharama ya shilingi milioni 347, na umejengwa kwa asilimia 70.
Wilaya ya Kyerwa Mhe.
Massawe alikagua mradi wa Maji Rwabikagati uliokamilika kwa asilimia 80 na
utagharimu zaidi shilingi milioni 880. Katika Wilaya ya Karagwe Mhe. Massawe
alitembelea na kukagua mradi wa Maji Chanika uliokamilika kwa asilimia 70 na
utagharimu shilingi milioni 734 ukikamilika.
Baada ya kutembelea na
kukagua miradi hiyo ya maji Mkuu wa mkoa alitoa maagizo kwa Wakandarasi wa miradi hiyo kuhakikisha miradi
hiyo inakamilika kwa wakati ili lengo la serikali litimie kwa wananchi kwa kupata huduma ya maji safi na salaama ifikapo 2015.
Mhe. Massawe pia
aliagiza baadhi ya Kamati za maji ambazo ziliundwa na hazitekelezi majukumu
yake ipasavyo zivunjwe na kuundwa upya ili kuleta ufanisi katika kuhaklikisha
miradi ya maji inafanya kazi na kutunzwa kama inavyotakiwa.
Aidha Mkuu wa Mkoa
alitoa agizo kwa taasisi za Serikali kuhakikisha zinalipa madeni ya ankara zao za maji kwani Taasisi hizo ndizo zinaongoza kwa Madeni
jambo ambalo linazifanya Mamlaka za Maji
kushindwa kujiendesha na kuimarisha huduma za maji kwa wananchi.
Angalizo, Mhe. Masswe
alitoa angalizo kwa wananchi miradi inakotekelezwa kuwa miradi hiyo itakapokuwa
imekamilika huduma haitatolewa mpaka pale wananchi watakapokuwa wamemaliza
kuchangia miradi hiyo ambayo wanantakiwa kuchangia asilimia 2.5 kwa kila mradi.
Imeandaliwa na:
Sylvester
Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2014
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment