Tazama picha chini baada ya basi hilo kunyanyuliwa upande mmoja
![]() |
| Gari hilo likionekana upandeni |
![]() |
| Basi hilo kwa mbele |
Basi la
timu ya Young Africans lililokuwa limebeba wachezaji pamoja na viongozi wa
benchi la ufundi limepata ajali eneo na Mikese Mizani mkoani Morogoro baada ya
Mabasi yaliyokua yakitanua kuelekea mikoa ya bara kuziba njia na kusababisha
kutumbukia kwenye mtaro.
Basi hilo
limepata ajali likitokea mkoani Morogoro kwenda Dar es Salaam baada ya mchezo
wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri,
Morogoro jana.
Taarifa
zinasema Katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa tatu na nusu asubuhi hakuna
mtu yeyote aliyejeruhiwa na kwa sasa timu inaondoka na usafiri wa basi jingine
kuelekea jijini Dar es salaam.


No comments:
Post a Comment