Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mmoja wa wafanyakazi katika hlamashauri ya manispaa ya Bukoba, Bwana Limbakisye Shimwela aliyekuwa mkurugenzi wa manispaa hiyo kwa muda wa miezi kadhaa amehamishiwa Dar es salaam.
Taarifa zinasema kuwa amehamishiwa Dar es salaam kupangiwa kazi nyingine ambayo hatahivyo haijajulikana na kuwaacha wafanyakazi wengine katika manispaa hiyo bila uhakika wa kazi yao kwani huyu ni mkurugenzi wa tatu kuondolewa Bukoba katika kipindi kifupi baada ya kutokea mgogoro wa utekelezaji wa miradi manispaa ya BUKOBA.
Kahmis Kaputa aliondolewa baada ya kutokea mgogoro mwanzoni mwa mwaka jana, Trazias Kagenzi akitokea Arusha akaondolea muda mfupi baada kufika Bukoba, na huyu ambaye ameingia katika nafasi hiyo katikati ya mwaka jana ameondolowa.
Endelea kufuatilia undani kupitia hapa.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment