![]() |
| Ni baadhi ya wananchi wakitafuta majina katika vituo vya kupigia kura. |
![]() |
| Baadhi ya Wanakijiji cha Kalenga A,kata ya Kalenga Iringa Vijijini mkoani Iringa wakiendelea kupiga kura kumchagua Mbunge wamtakaye wa jimbo hilo la Kalenga. |
![]() |
|
Baadhi ya akina Mama waliojitokeza
kupiga kura mapema leo asubuhi katika kijiji cha Kalenga A,kata ya Kalenga
Iringa Vijijini wakitazama majina yao kwenye ukuta tayari kwa kutumia haki yao
ya msingi ya kumchagua kiongozi wamtakae kwa kupiga kura
|
Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo unafanyika
leo,ambapo vyama Vitatu;CCM,CHADEMA na CHAUSTA vikiwa vimesimamisha wagombea
wake katika uchaguzi huo unaotokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo
hilo,pia Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa.
Aidha Wagombea wa Chadema Grace Tendega
na wa CCM,Godfrey Mgimwa ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kuchuana na hatimaye
mmoja wao kuibuka kinara kwa kupigiwa kura na Wananchi,huku mgombea wa
CHAUSTA,Richard Minja akipewa nafasi ndogo kutokana na maandalizi hafifu ya
ushiriki wake.
Na Mwanaharakati.




No comments:
Post a Comment