MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 15 March 2014

MBARONI KUKUTWA NA SARE ZA JESHI


Anasema “Mdogo wetu Omari alikuja nyumbani na kutuambia amekutana na mtu anayehusika na fomu za kujiunga na Polisi na kwamba zinauzwa kwa shilingi 250,000. Kwa kuwa hakuwa na hela, aliamua kuuza kitanda na godoro na fedha zingine akaongezewa na mama,” alisema mmoja wa dada wa kijana aliyetapeliwa, aliyejitambulisha kwa jina la Siwa.

Alisema baada ya kupata kiasi hicho, Omari alimfuata mtu huyo akiwa na rafiki yake aitwaye Ali Kassimu ambaye naye alitaka kununua fomu hiyo.

Baada ya kumpatia, walipewa fomu hizo na kuelezwa kuwa walitakiwa kusafiri kuelekea Tanga sehemu iitwayo Kibuku ambako ndiko ilipo kambi yao.

Walipofika huko, waliulizwa kuhusu zilipo fomu za kujiunga, lakini walipowaonyesha, askari waliokuwepo kambini hapo walizibaini kuwa hazikuwa halisi, hivyo vijana hao waliwekwa chini ya ulinzi ili kusubiri taratibu zingine kufuatwa.

Ni kwa hisani ya EDDY.

No comments: