Watanzania wane akiwamo mwanamume mmoja na wanawake watatu, wamekamatwa na dawa za kulevya aina ya HEROIN kilo 2.2 kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenya JOMO KENYATA(JKIA).
Tarifa zinasema kuwa watanzania hao waliingilia mpakani Namanga
wakielekea HONG KONG nchini China.
Msemaji wa polisi katika uwanja huo, amesema kuwa, “tumewakamata
watanzania wane na tumewaweka chini ya uangalizi mkali, wameshatoa kete
(vidonge) 186 ambazo tumezifanyia uchunguzi na na kudhibitisha kuwa ni heroin”
Ngisa pia aliliambia shirika la habari la China XHINUA kwa njia ya simu.
Amesema kuwa upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani
mara moja.
Na Mwanaharakati.

No comments:
Post a Comment