![]() | |
Moja ya nyumba zilizooezuka. |
![]() |
Baadhi ya mabati yaliyopeperushwa na upepo |
![]() |
Ni nyumba mojawapo iliyoezuka paa na baadhi ya kuta kudondoka. |
Zaidi ya mashamba 100 ya migomba katika kijiji cha
bulembo kata ibuga wilayani muleba yamealibiwa na mvua iliyonyesha leo
ikiambatana na upepo mkali.
Alikadhalika kufuatia mvua hiyo nyumba 15 zimeezuliwa
na upepo katika kisiwa cha Musira kilichoko manispaa ya bukoba.
Akizungumza na kasibante fm redio mwenyekiti wa kisiwa
hicho bwana CHALES POLEPOLE ameeleza kuwa sambasamba na kuezuliwa kwa nyumba
hizo pia mtu mmoja amejeruhiwa vibaya baada ya kuangukiwa na ukuta wa
nyumba,huku miti na migomba pia ikivunjwa na upepo huo.
No comments:
Post a Comment