Umemalizika sasa wilayani Temeke na unarushwa live kupitia ITV Radio One na TBC 1, ambapo Abdulrahman Kinana ambaye ni katibu mkuu wa CCM, amesema vyama vya upinzani vinataka serikali tatu ili vishinde.
Kauli hizo za CCM , zinakuja katika kipindi ambacho mchakato wa katiba unalalamikiwa kutokana na misimamo ya vyama vya siasa pasipokujali watanzania, jambo ambalo linaleta mvutano mkubwa bila kujadili masuala ya msingi bungeni.
Katika hotuba yake, rais Kikwete alionesha msimamo wake katika kuipata katiba mpya, jambo ambalo Kinana anasema limenukuliwa vibaya na linatumiwa ndivyosivyo na kuleta nongwa hapa nchini.
Katika mkutano huo mwenyekiti vijana wilaya Temeke na katibu wa CHADEMA Temeke, pamoja na wanachama wengine wa chama hicho.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment