Waziri
mkuu Pinda akiweka udongo kwenye kaburi, hapo Kilosa
Waziri mkuu Pinda akimfariji mzee
Gabriel Tupa, baba mzazi wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara John Gabriel Tupa,
baada ya mazishi.
|
Bwana TUPPA alifariki ghafla Machi 25,
mwaka huu, akiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime, JOHN HENJEWELE,
wakati akipokea taarifa ya wilaya ambapo alitarajiwa kuweka jiwe la msingi
katika jengo la kusaidia matatizo ya ardhi na kushiriki ufungaji wa mafunzo ya
mgambo.
Mwili wa marehemu Tuppa,uliagwa jana na
maelfu ya wananchi wa mkoa wa Dodoma kabla ya kuelekea KILOSA, mkoani Morogoro kwa
ajili ya mazishi.
Wakati wa uhai wake, marehemu Tuppa
aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya za Chunya, Mwanga, Bukoba, Muleba na Dodoma, kabla
ya kupandishwa cheo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara mwaka 2011.
Marehemu Tuppa alizaliwa Januari mosi,
1950 wilayani KILOSA, mkoani Morogoro, ameacha Mjane na Watoto Watano.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment