STAA wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amepata
ajali ya gari wakati akielekea Loliondo, Arusha kupata dawa ya kikombe
inayotolewa na mchungaji mstaafu, Ambilikile Mwaisapila.
ude ameiambia Bongowood kuwa, hivi
karibuni walikuwa na gari aina ya Toyota Prado wakimpeleka mama yake kupata
tiba ya ganzi mwilini ndipo tairi lilipopasuka na gari kuangukia gema.
“Ilipoteza muelekeo, likayumba lakini nashukuru Mungu hatukuumia, tukasaidiwa kunyanyua, tukaenda kupata tiba ya babu,” alisema Dude.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment