MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 24 March 2014

KAYA 56 ZAATHIRIKA NA MVUA BUKOBA; SEHEMU YA VIDEO IKO HAPA

Ni maafa yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia leo ambapo katika mitaa mbalimbali ya kata za bakoba na Kitendaguro migomba na nyumba za kaya zaidi ya 60, zimeharibiwa vibaya. (Video hiyo hapo juu inaonesha moja ya kaya zilizoathirika.)
Ni nyumba ya David Joseph ambaye ameangukiwa na nyumba hiyo na kujeruhiwa ambapo amepelekwa hospitali ya mkoa kwa matibabu baada ya mkono kujeruhiwa na kutoa damu puani.

Ni nyumba ya mzee Paul Phinkili imeezuka na magodoro mengine yameanikwa wakati nikifika katika eneo hilo.

Ni baadhi ya migomba iliyoangushwa na upepo


Hapa yupo mama mjane Bi Suzan Mutalemwa nyumba na migomba picha hii ni jiko lote limesambaratika.

Picha hii inaonesha waya wa umeme umekatika na lakini watu hawakujeruhiwa na juhudi za Tanesco zinaendele.

Hata miti nayo imekumbwa katika mvua hizo ikiwamo mipera ovakado na mihumura

Huu ni mti wa mbao ulivyong"oka na upepo




No comments: