MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 6 March 2014

MAKAMU WA RAIS KUZINDUA HUDUMA ZA MSD MULEBA

 Ni tarehe 8 mwez huu wilayani Muleba mkoani Kagera, ambapo huduma za Bohari kuu ya dawa inazinduliwa ili kuhudumia mikoa ya Kagera na Geita.
 Pamoja na uzinduzi huo, makamu wa Rais Dk GHARIB BILAL, atafungua sherehe za maadhimisho ya siku ya akina mama duniani, itakayofanyika wilayani Muleba kimkoa.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Kagera, mkuu wa mkoa huo FABIAN MASSAWE, amesema kuwa makamu wa riais atawasili kesho mach 7 2014, na uzinduzi pamoja na sherehe vitafanyika 8 mach 2014 katika wilaya ya Muleba ambapo sherehe za akina mama duniani zitafanyika katika uwanja wa FATUMA.
 Pamoja na ujio huo, mkuu wa mkoa amewaomba wananchi kuudhuri na kuupokea mwenge wa uhuru mwezi April mwaka huu, utakaowashwa mkoani Kageara ktika manispaa ya Bukoba ambapo amesema kuwa harakaili zimeshaanza kufanyika katika uwanja wa Kaitaba manispaa ya Bukoba.
 Picha juu Rc Massawe akiongea na waandishi habari na chini ni waandishi habari wakisiliza kwa makini maneno ya mkuu wa mkona ambaye amesema kuwa leo naibu waziri wa afya atawasili mkoani Kagera.
Na Mwanaharakati.

No comments: