
Bi. Mwanaidi Athumani mkazi wa
Chamwino Morogoro hivi karibuni alifanya mchepuko wa kutoka nje ya ndoa na
kujikuta akijifungua mtoto wa kiume ndani ya gesti iliyopo maeneo ya Mafisa
mjini hapa
Habari zinasema kuwa mwanamke huyo
alifanya mchepuko huo baada ya mumewe kusafiri kwenda kutafuta fedha za
maandalizi ya kujifungua kwake.
Bila ya kujali kama ana mimba ya
miezi saba, Mwanaidi aliingia katika gesti moja (jina tunalo) akiwa na mwanaume
anayedaiwa kufanya kazi ya kupiga debe katika stendi ya Msamvu na mambo
yalipomwendea kombo, mwanaume huyo akatimua mbio.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, Mwanaidi
na mpiga debe wake walipanga katika chumba namba 3 na baada ya kufanya mambo
yao, Mwanaidi akaanza kupiga kelele kutokana na kushikwa na uchungu. Ilimbidi
mhudumu wa gesti hiyo, Bi. Moshi Eliya afike kumsaidia Mwanaidi aweze
kujifungua salama pamoja na kwamba hakuwa na ‘gloves’ wala kitu chochote cha
kulinda afya yake.
Chanzo chetu ambacho nacho kilikuwa
ni mpangaji ndani ya gesti hiyo kilisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 8 usiku
na Mwanaidi alipiga kelele huku akizozana na mpiga debe wake. Kiliposikia tukio
hilo, chanzo hicho kikapiga simu kwa paparazi wetu aliyetinga katika nyumba
hiyo ya wageni kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo.
Baada ya kujifungua salama, paparazi
wetu alimuuliza Mwanaidi kilichotokea ndipo mwanamke huyo akafunguka kuwa
alikuwa amechepuka nje ya ndoa baada ya kukumbwa na shetani.
“Nina mume na tuna watoto watatu
huyu ni wanne, mume wangu amesafari kwa ajili ya kutafuta fedha za maandalizi
ya ujuo wa mwanetu akijua nina mimba ya miezi saba,” alisema mwanaidi.
Pamoja na kutaka kugoma, lakini
mwandishi wetu alimchukua mwanamke huyo na kichanga chake na kuwapeleka
Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambako wamelazwa kwa uchunguzi zaidi.
Mhudumu wa gesti hiyo, Bi. Moshi
Eliya ambaye alikuwa mkunga wa Mwanaidi alisema kuwa alishindwa kutumia
‘gloves’ wakati wa kumzalisha mzazi huyo kwa kuwa alikumkuta mtoto ameshaanza
kutoka. “Mtoto aliashaanza kutoka, hata hivyo kwa usiku ule tungepata wapi hizo
gloves?” alihoji.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment