MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 23 March 2014

MTALII ALIYEKWAMA KILIMANJARO AOKOLEWA

 Ameokolewa baada ya taarifa rasimi kufika maeneo husika
Mtalii Jeanne Traska kutoka Ujerumani

Bi.Jeanne Traska kutoka Ujerumani na Muongoza Wageni Athumani Juma wakiwa katika Lango la Marangu pamoja na vifaa mbalimbali walivyokwama navyo katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro mara baada ya kuokolewa.

Uokoaji katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro kimefanikiwa kumuokoa mtalii Bi. Jeanne Traska (32) kutoka Ujerumani pamoja na muongoza wageni Athuman Juma ambao jana walikwama katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro. Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kufika eneo la
kilele cha Mawenzi na kwa kutumia mbinu za uokoaji za kisasa kabisa kiliweza
kuwanasua majira ya kumi na moja jioni.


Licha ya hali mbaya ya hewa iliyotokana na mawingu mazito katika eneo hilo, Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kukabiliana na hali hiyo na kuweza kuwanasua na kisha kuwapeleka katika kituo cha Horombo majira ya saa mbili usiku ambapo walichukuliwa na gari kupitia njia
maalum ya uokoaji na kufika katika Lango Kuu la Marangu saa nne na nusu usiku.


Hali ya hewa ilisababisha helikopta maalum iliyoletwa kwa ajili ya zoezi la uokoaji kushindwa kufanya kazi kwa kuwa mawingu mazito hayakuwezesha marubani kuliona eneo la kilele kwa urahisi.

Hivi sasa mtalii huyo pamoja na muongoza wageni wake bado wapo chini ya uangalizi wa hifadhi kwa kushirikiana na Kampuni ya Nordic Tours iliyomleta mgeni huyo.

Aidha, kwa kuwa ni tukio lisilo la kawaida, uongozi wa hifadhi unaendelea kuchunguza sababu zilizowafanya kuchepuka njia na kuelekea kilele cha Mawenzi badala ya Kibo. Kwa kawaida
Kilele cha Mawenzi huwa hakitumiwi na watalii isipokuwa kwa kujaza fomu maalum
inayoonyesha kuwa mgeni amekubali kwa hiyari yake kupanda kilele hicho.

Imetolewa na Idara ya Mawasiliano

Hifadhi za Taifa
Na Mwanaharakati.

No comments: