Hiyo imebainika katika taarifa Timu ya
Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya
ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa ukarabati na upanuzi wa mitambo hiyo iliyopo
mkoa wa Pwani.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mhandisi
Deusdedit Rwegasira na Mhandisi Emmanuel Makusa ambao ndiyo wasimamizi wa
mitambo hiyo, walisema kuwa hali ya ukarabati wa mitambo hiyo inakwenda kwa
kasi na inatarajiwa kukamilika kwa wakati, hivyo kutoa ishara njema ya kumaliza
tatizo sugu la maji kwa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Mafundi wakiendelea kulaza mabomba yatakayotumika
kusafirishia maji kutoka Mitambo ya Maji ya Ruvu Chini mpaka kwenye Tanki la
kuhifadhia maji lililopo Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa
mafundi hao wameshasambaza mabomba kwa umbali wa kilomita takribani 29 kati ya
kilomita 55. Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, mwaka huu.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango ikikagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa mitambo
ya Ruvu Juu ilipofanya ziara ya ukaguzi katika Mtambo huo uliopo mkoa wa Pwani.
 |
Meneja wa Mtambo wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel
Makusa (Kushoto) akiwaonesha Wataalamu wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango mashine nne mpya zilifungwa na Serikali hivi
karibuni walipofanya ziara ya ukaguzi katika Mtambo huo uliopo mkoa wa Pwani.
|
 |
Viongozi wa msafara wa wataalam wa ukaguzi wa
miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Naibu Katibu
Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri
(Wapili Kushoto) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus
Rutasitara (Watatu Kulia) wakionesha eneo la kusafishia maji katika Mtambo wa
Ruvu Chini walipokuwa katika ukaguzi wa mtambo huo. Kushoto ni Mratibu wa ziara
hiyo, Bibi Salome Kingdom.
|
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment