Abas Kinzasa ‘20%’, anadaiwa kunaswa
laivu akiwa kwa mganga wa kienyeji akipata tiba ya kupunguza na kuondoa sumu ya
utumiaji wa bangi na pombe
Ni katika kijiji cha Ngukumo mkoani
Tabora baada ya mameneja wa wasanii wa Bongo Fleva, Papa Misifa na Steve Mbaga
kumshika mkono 20% na kutafuta mganga wa kienyeji ambaye aliwatangazia kuwa ana
dawa zinazoweza kumuondoa sumu hiyo.
Mameneja hao ambao walisema
walilazimika kufanya hivyo ili waweze kumrudisha 20% kwenye gemu kwa mara
nyingine kwani bado wanaamini ana uwezo mkubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva.
“Kiukweli mimi na mwenzangu tumekuwa
tukisikitishwa kwa muda mrefu baada ya 20% kubobea kwenye matumizi ya pombe na
bangi na hasa alipozidiwa hadi akashindwa kufanya muziki huu ambao tunaamini
kwake ndiyo ilikuwa ajira pekee.
“Kwa kutambua hilo tulimtafuta na
kuongea naye, alipokubaliana nasi tukaamua kumpeleka kwa mganga wa kienyeji,
ameshapata tiba na tayari ameonyesha kujitambua, hivyo hivi karibuni tunaanza
kufanya naye kazi na ndiyo tunatoka kumlipia nyumba ya kuishi maeneo ya Mwananyamala
Hospitali,” alisema Papa Misifa.
Kupitia (Ijumaa Wikienda) nilipopata
story hii, lilimtafuta 20% ambaye mwaka 2011 alichukua tuzo tano za Kili alipozungumzia
suala hilo “Ni kweli Papa Misifa na Steve Mbaga wamejitahidi sana kunifanya
niachane kabisa na matumizi ya pombe maana walinipeleka kwa mganga wao ambaye
kweli amenisaidia.
“Ujue kilichokuwa kikiniyumbisha
siku zote hizo ilikuwa ni pombe maana bangi ilikuwa si kiivyo, nilipokuwa
nakunywa pombe kweli ilikuwa ikinitoa kwenye njia na kunifanya kujiona mimi
ndiyo mimi kiasi cha kushindwa hata kuwaheshimu wenzangu na ndiyo jambo pekee
ninaloweza kusema limenifanya kuwa hivi.”
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment