MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 14 April 2014

ASKARI POLISI ANASHIKILIWA KWA KUGONGA WATU AKIWA AMELEWA


Mkuu wa kituo cha Polisi Kahama Elias Haway

Haway alipohojiwa amekiri kutokea kwa ajali hiyo huku alisema kuna upotoshaji mkubwa wa taarifa hiyo kwani yeye ndiye aliyegongwa na mwendesha pikipiki huyo wa kwanza. 

Amesema alipotaka kusimama kumwona mtu huyo aliyegonga,  aliona watu wameanza kumzonga naye akamua kukimbia kwa usalama wake ndipo alipoweza kuwagonga tena wale wengine wawili.

Mganga Mfawidhi wa Hospitari ya wilaya ya Kahama Dk Joseph Foma amethibitisha kugongwa na gari watu hao na wamelazwa katika wodi namba moja katika hospital hiyo, huku hali zao zikiwa mbaya na kwamba wapo katika utaratibu wa kumuhamishia Malugu katika hospitali ya Bugando Jijini Mwanza.



Msukuma Toroli Fitina Majuto akiwa Hospitalini Hapo

  Mtembea kwa miguu Cosmas Peter akiwa hoi hospitalini

Ajali hiyo imetokea Jana majira ya 1.30 usiku katika barabara itokayo isaka kuingia kahama mjiniu ambapo Haway akiendesha gari yake Toyota  Rav 4  lenye namba T 798  BSK alimgonga mwendesha pikipiki. 

Watu waliogongwa wametambuliwa kwa majina ya Joseph Malugu (35) mkazi wa Mbulu  Bw. Fitina Majuto (20) na Cosmas Peter (21) wote wakazi wa mjini hapa mitaa ya  Nyasubi mjini Kahama. 

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema Haway alianza kumgonga mwendesha bodaboda Bw. Malugu katika eneo la Zahanati ya Igalilimi  ambapo watu  wenye hasira  walimzingira wakimtaka asimame naye akakimbia huku akiwagonga tena  waenda kwa mguu wawili.

Wamesema Haway akionekana kuwa amelewa hakutaka kuwatii  watu  waliyokuwa wakimweleza  ndipo alipoondoa  gari lake   kwa mwendo kasi   na  kwenda kumgonga   Bw. Majuto katika   eneo la  Mkude  ambae aliumia sana kwenye sehemu ya tumbo na kusababisha utumbo kutoka nje.

Shuhuda mmoja  Mkulo Iddy amesema eneo hilo pia Haway hakutaka kusimama na aliendelea na mwendo kasi ndipo alipokwenda kumgonga mtu mwingine  wa tatu   Bw. Peter katika barabara  ya eneo la Paradise mitaa ya Nyasubi.

Na Mwanaharakati.

No comments: