![]() |
| Askari wakiangaika kuwasha pikipiki iliyomgongwa mama mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa. |
![]() |
| Mama aliyegongwa akipatiwa huduma ya kwanza na wasamalia wema baada ya askari kutomjali. |
![]() |
| Kulia ni askari magereza aliyemgonga mama huyo katika manispaa ya Bukoba, na kushoto ni mmoja ya wasamalia wema aliyempeleka mama kupatiwa matibabu. |
Baada ya askari wa kama kamata pikipiki manispaa ya Bukoba kufika muda mfupi baada ya tukio hilo, walikuta mama huyo akigaragara, wao wakakimbilia kukamata pikipiki na kuipeka kusikojulikana badara ya kutoa huduma ya kwanza kwa huyo majeruhi kwani aliyemgonga hakua na jinsi na wala hakuwa na nia ya kukimbia bali alikuwa akiomba msaada.
Kumekuwa na desturi ya kukamata wafanyabiashara ya kubeba abiria, ambapo yameshajitokeza malalamiko kuwa wanawakimbiza katika mazingira hatarishi, ilihali wakiwatoza fedha zisizo na vithibitisho au stakabadhi.
Na Mwanaharakati.



No comments:
Post a Comment