![]() |
| Rais Jakaya Kikwete akizungumza kwenye uzinduzi wa kongamano la 19 la mwaka la utafiti liliandaliwa na taasisi ya utafiti nchini REPOA. |
“mpaka ukifika mwezi Oktoba basi sheria na taratibu zote zitakuwa tayari na kufungua milango pia kwa wawekezaji wa ndani kushiriki kwenye sekta ya gesi na mafuta nchini,”
Amesema kwamba kwenye uwekezaji wa gesi na mafuta taifa litapata manufaa makubwa na mabilioni ya pesa yataingia kwa hiyo ni nafasi muhimu pia kwa watanzania wenye biashara za kati na ndogo ndogo kunufaika na uwekezaji huo.
Rais Kikwete alisisitiza kwamba katika uwekaji wa sheria na taratibu lazima mambo ya urasimu na rushwa viondolewe mara moja ili kuhakikisha sekta hiyo inakuwa na manufaa kwa wananchi wote.
Aliongeza kwamba lazima serikali na wadau wote muhimu wajiridhishe kwamba hakuna wizi wala utapeli katika sekta gesi na mafuta ili kumletea mwananchi wa kawaida maendeleo.
Kikwete alifafanua kwamba lazima serikali ihakikishe inajipanga vizuri ili kuzuia vitendo vyovyote vya hujuma, wizi na rushwa ili kuleta matokeo chanya kwa nchi na watu wake.
Amesema kwamba kwa muda mrefu watafiti wa ndani wamekuwa na msaada mkubwa katika kuisaidia serikali kutambua maeneo yenye mahitaji zaidi na hasa katika kuboresha maisha ya wananchi na kupambana na tatizo la ajira nchini.
aliongeza“tafiti hizi za kila mwaka zimekuwa na msaada mkubwa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo, wakulima na wananchi wa kawaida katika kufanya uamuzi sahihi kwenye maeneo,”
Amesema kwamba nchini Tanzania zipo ajira ndogo ndogo milioni tatu lakini wanaofanya ajira hizo ni milioni tano na laki mbili kati hao asilimia 64 ni wanawake.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA, Profesa Samwel Wangwe amesema kwamba tafiti hizi zinalenga kuwasaidia wananchi wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo ili kupunguza umaskini.
Profesa Wangwe amesema kwamba malengo ya tafiti pia ni kuongeza tija kwa kupata uzoefu kutoka nchi mbalimabali ulimwenguni ya jinsi ya kujenga viwanda, kusindikaji wa chakula na kupambana na tatizo la ajira hasa kwa vijana na wanawake.
Aliongeza pia kwamba REPOA wamewaalika wataalamu mbalimbali kutoka nchini ya Japan ili watanzania waweze kujifunza kutokana na nchi zao katika harakati za kupambana umaskini Afrika.
Na Mwanaharakati.


No comments:
Post a Comment